![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjqQN7BsikUF1Z_YVlMVnjX8KEeLugutASoi5KxJE5exajJnjMcIWGQoLLkO40VhDJpiRQvTe3sMv4ywWANDE86Vdb7PjqaPdbm89ncjvQTquGfC80P5QEpldEGM1xVeVn4LFf0qauFEaKQ/s400/30-01-2010.jpg)
Kwa niaba ya uongozi mzima wa Jumuiya ya Watanzania Rome, napenda kuwashukuru wanajumuiya wote wa Jumuiya ya Watanzania Rome kwa mshimano mliouonyesha kwenye kipindi hichi cha mwaka 2011. Jumuiya ya Watanzania Rome, ambayo ina miaka miwili tokea kuanzishwa kwake, imeweza kufanya mambo mengi sana ambayo yameweza kuwapendeza watu wengi na imeweza pia kujipatia sifa nyingi kutoka kwa wadau mbalimbali dunia nzima.
Mimi kama katibu na mwanzilishi wa hii blog napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wale wote waliotembelea blog hii tokea nilipoianzisha na kunipa ushauri mzuri ambao ndio umeiwezesha blog hii kuwavutia watu kila kona ya dunia.
Kazi ya blogging, si kazi rahisi kama wengi wanavyofikiri. Ni kazi ambayo inaitaji utumiaji wa muda mwingi wa kutafuta habari na picha mbalimbali na kisha mpangilio mzima wa hizi picha na habari. Ni vyema kabisa nimshukuru mwenyezi mungu kwa kunipatia ujuzi na mwongozo kwenye kuiendesha blog hii. Pia niwashukuru wadau pia kwa uzalendo wenu kwenye kuisimamissha blog hii.
Napenda pia kuwaomba radhi wadau wote wa blog hii kwa kunivumilia pale ambapo blog ilipopata kwikwi kwa kipindi flani kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wangu.
Ombi langu kwenu wadau kwa mwaka mpya 2012 ni moja tu. Ili blog izidi kusimama vizuri zaidi, naomba ushirikiano wenu uendelee kwenye kunitumia habari na mapicha mbalimbali, maana mara nyingi kwenye nguvu zaidi ya moja mambo uenda vizuri zaidi.
Mungu Ibariki Africa, Mungu Ibariki Tanzania na Mungu tubariki Wanajumuiya wote wa Jumuiya ya Watanzania Rome.
wenu,
Andrew Chole Mhella
Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Rome.
Blogger!
No comments:
Post a Comment