

ROME: Timu ya mpira wa miguu ya AC MILAN jana ilifanikiwa kuunyakua ubingwa wa Italia baada ya miaka 7. AC Milan ambayo ilikuwa inaitaji kupata point moja tu kwenye mechi tatu zilizobakia ilitoa droo ya 0-0 na timu ya Roma na hivyo kuinyakua point moja ambayo iliwafanya washangilie ubingwa huu wa Italia. Itakumbukwa kuwa timu ya AC Milan kwenye kipindi cha usajili wa wachezaji walinunua wachazaji machachali kama vile Ibrahimovic, Robihno, Boeteng, Cassano, Van Bommel na Emmanuelson ambao walichangia kwa kiasi kikubwa kuiongezea timu hii ukali. Baada ya mechi hii, Mmiliki wa timu Silvio Berlusconi amewaaidi mashabiki na kocha kuwapatia zawadi kubwa ya wachezaji mashuuri dunia ambao hakuwasema lakini dalili zipo wanunua wachezaji kama vile Cristiano Ronaldo wa Real Madrid, Bale wa Tottenham au Essien. Yetu macho tukae mkao wa kula tusubilie kipindi cha ununuzi utakapo anza.
No comments:
Post a Comment