Madau wa blog ya Jumuiya ya Watanzania Roma Ndg. Andrew Kyabashasa ameibukia Haiti kama inavyoonekana katika picha alizotutumia. Ikumbukwe tulimuaga Ndg. Kyabashasa mwanzoni mwa Disemba 2010 lakini hakueleza alikuwa anaelekea wapi. Amewatakia Wanajumuia maandalizi mema ya sikukuu ya Muungano na maonyesho ya utamaduni wa Mtanzania.Basi na sisi kama Jumuiya ya Watanzania Roma, tunachukua nafasi hii kututakia mafanikio mema huko ulipo na kukukaribisha sana kwenye sherehe zetu za mwezi wa nne hapa mjini Roma.

Mdau Andrew Kyabashasa na background ya picha ni makazi ya muda ya wenyeji baada ya tetemeko la January 12, 2010

Jinsi wajenzi wa Haiti walivyo na kazi pevu ya kujenga milimani
Safi sana Mjumbe! wasalimie wajombi huko Kwa Aristide!
ReplyDelete