
UMOJA CHA WANAFUNZI WAKATOlIKI WATANZANIA ROMA, kinayofuraha kuwakaribisha watanzania wote kwenye ANNIVERSARY ya kifo cha Baba Wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere pale (Collegio San Pietro)San Peters College iliyopo kwenye mtaa wa Via Mura Aurelie 4 mjini Rome. Itakumbukwa kuwa Baba wa Taifa alifariki tarehe 14 Oktoba 1999 mjini London kwenye Hospital ya San Thomas na anniversary ilikuwa ifanyike tarehe 14 Oktoba, lakini kutokana kutowezekana kufanyika tarehe hiyo Chama cha Wanafunzi Wakatoliki Watanzania Roma, kimeamua kuadhimisha jumapili ya wiki hii tarehe 24/10/2010. Adhimisho litaanza na misa saa tano asubuhi na kufuatana na chakula cha mchana. Kwa Wanajumuiya wote mnaopenda kushiriki mnaombwa muwasiliane na katibu wa Jumuiya ya Watanzania Rome kwa e-mail hii ya jumuiya.watanzaniaroma@yahoo.it.
No comments:
Post a Comment