Umoja wa Wanafunzi Wakatoliki Watanzania Roma pamoja na baadhi ya Wanajumuiya wa Jumuiya ya Watanzania Rome, wakiongozwa na ujumbe maalum toka kwa Mwenyekiti Mh. Leonce Uwandameno na Mwenyekiti msaidizi Mh. Erasmus Pindu Luhoyo, walijumuika pamoja
collegio San Pietro asubihi ya leo (24/10/2010) Kushiriki kwenye Misa Takatifu ya kumuombea Baba wa Taifa kwenye adhimisho lake la miaka kumi na moja (11) tokea kifo chake na kuiombea Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu wa Tarehe 31 Oktoba 2010.Shughuli nzima ilianza na misa mnamo saa tano asubuhi ambayo iliongozwa na
Baba ASKOFU wa Jimbo Katoliki la Tunduru-Masasi, CASTOR PAUL MSEMWANA na baadae kufuatiwa na chakula cha mchana.
Tokea kushoto ni Baba Askofu Castor Paul Msemwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Rome, Mh. Leonce Uwandameno na katikati ni mwenyekiti wa Umoja wa Wanafunzi Wakatoliki Roma, Fr. Nicodemus Hindoy.
Mjumbe wa Jumuiya ya Watanzania Roma, Dr. Boniface Mhella akipata picha ya Pamoja ya ukumbusho na baba Askofu pamoja na viongozi wa Juu wa Jumuiya za watanzania.
Wakati wa Misa ya kumuombea Baba wa Taifa pamoja na kuiombea Tanzania kwenye uchaguzi Mkuu wa tarehe 31 Oktoba 2010.
Naitwa Malkiory William Matiya,ningependa kuwasiliana na Fr. Nicodemus Hindoy ambaye nilikutana naye kwa mara ya kwanza Mlale JK mwaka 1991. Ilikuwa ikiitwa Operesheni miaka 30 ya Uhuru. Kwa kweli ni muda mrefu sijapata kuonana wala kuwasiliana naye japo tulikuwa wote hodari kwa kilimo pale jeshini Mlale Songea. Kwa yeyote mwenye mawasiliano yake naomba aniandikie kwa email ifuatayo: malkiory@gmail.com
ReplyDelete