Mh. Mohamed Shein

Mh. Balozi Ali Abeid Karume
Zoezi la Kumpata mgombea urais Zanzibar kupitia chama tawala cha CCM limekamilika leo ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dr. Mohamed Shein ametoka kidedea kwa kupata ushindi mnono wa kura 117. Wagombea wengine wa CCM visiwani Zanzibar, Mh. Bilal alipata kura 54 na Mh.Nahodha kura 33. Washiriki wengine ambao walikuwepo kwenye kinyang'anyiro hicho ambapo mmoja wao alikuwa ni balozi wa Tanzania nchini Italy, Mh. Ali Abeid Karume,walishindwa kupata nasafi hiyo kwa kipindi hiki cha uchaguzi 2010. Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania Rome kwa niaba ya wanajumuiya wake wote, unampongeza Mh. Dr. Mohamed Shein kwa kupata nafasi hii ya kugombea kupitia Chama cha Mapinduzi kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu utakao fanyika mwezi wa kumi na kuwapongeza pia wagombea wengine akiwemo balozi wetu hapa Italy Mh. Ali Abeid Karume kwa kuwa mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo. Itakumbukwa kuwa Jumuiya ya Watanzania Rome ni Jumuiya ambayo si ya Kisiasa lakini pia ni muhimu sana kuwapongeza viongozi wetu bila kujali vyama vyao vya siasa pale wanapopiga hatua ya kuleta maendeleo nchini Tanzania. Hii yote inaonyesha ukuaji wa demokrasia nchini Tanzania. Mungu Africa, Mungu Ibariki Tanzania.
No comments:
Post a Comment