Mh. Balozi akitoa ushauri wake kuhusu maswala ya Jumuiya.
Jana tarehe 4 mwezi wa saba mjini Roma, ulifanyika mkutano mkuu uliokuwa na lengo la kufungua Tawi la Jumuiya ya Watanzania Roma. Mkutano huu uliudhuliwa na mgeni rasmi ambaye alikuwa Mh. Balozi A. Karume. Mkutano ulikuwa na agenda zifuatazo: kwanza kabisa kupata ufafanuzi wa Katiba kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio Italy; kupata ufafanuzi wa ufanyaji kazi wa Jumuiya ya Watanzania Italy, na mwishoni ni kufanya uchaguzi wa Kuwachagua viongozi wa Jumuiya ya Watanzania waishio Roma. Uchaguzi ulienda vizuri na waliochaguliwa kwenye Vyeo hivi ni MWENYEKITI (Bi. Zuhura), KATIBU (Mr. Andrew Mhella) na MWEKA HAZINA(Mr. Awadhi). Uongozi huu ungependa kuwaomba ushirikiano ilikufanikisha malengo yetu kwa pamoja. Hizi ni baadhi ya picha za shughuli hiyo ya jana, zingine zitafuata very soon.