Watanzania nchini Italia, Jumamosi tarehe 26 Aprili 2014, walikutana mjini Roma kwenye ukumbi wa Ubalozi uliopo Viale Cortina d’Ampezzo 185, kusherehekea sikukuu ya kuadhimisha miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Mgeni rasmi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Dkt. James A. Msekela. Sherehe ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Jumuiya za Watanzania Italia, Maofisa wa Ubalozi na familia zao, Maofisa wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyoko Roma na familia zao pamoja na Watanzania waishio Italia.
|
Hii ndio ilikuwa keki ya Muungano |
|
Bi. Mary Mtemahanji, mwakilishi wa Jumuiya ya Watanzani Modena akiimba kwa furaha wakati wa kufungua champeign. |
|
Bi. Zainab na Bw.Peter wakikata keki ya Muungano kwa pamoja. |
|
.
Picha ya pamoja. Kushoto ni Katibu wa Jumuiya wa Watanzania Roma na pia Katibu wa Kamati ya Diaspora Italia Bw. Andrew Chole Mhella, katikati ni Bw. Peter na kulia ni Mjumbe wa Jumuiya ya Watanzania Roma Bw. Kondela Buhire. |
|
Mheshimiwa Balozi Dkt. James Msekela akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Italia Bw. Abdulrahmani A.Ali. |
|
Kutoka kushoto ni Bw. Karim Msemo, Ofisa wa Ubalozi Roma; Bw. Peter na Bw. Kondela Buhire, mjumbe wa Jumuiya ya Watanzania Roma. |
|
Mh. Balozi akisalimiana na Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Roma na Katibu wa Kamati ya Diaspora Italy ndugu Andrew Chole Mhella. |
|
POZ KWA POZ |
|
Wadada |
|
Picha ya pamoja ya baadhi ya viongozi wa Jumuiya za Watanzania Italia na Ofisa wa Ubalozi. |
PICHA ZINGINE ZITAFUATA BAADAE.
( Picha zote zimepigwa na Ndugu Karim Msemo)
No comments:
Post a Comment