Wanajumuiya wa Jumuiya ya Watanania Roma, siku ya jumamosi tarehe 15 Machi walikutana kwenye Restaurant ya Kihindi iliyopo maeneo ya Termini kujadiri mwenendo mzima wa Jumuiya ikiwemo michango, urekebishwaji wa katiba, na zaidi kumshukuru na kumuaga Mr. Emsofi Meena ofisa wa ubalozi wa Tanzani Italy, aliyemaliza muda wake wa kazi ubalozini, kwa kuwa sambamba na Jumuiya tangu pale ilipoanzishwa! Mr. Meena alikuwa kama mlezi wa jumuiya maana alitupa mawazo ambayo yametusaidia kwa kiasi kikubwa kuimalisha Jumuiya yetu. Mwenyekiti aliwashukuru pia wanajumuiya kwa kuonyesha ushirikiano wao wa dhati, kwenye misiba inayowapata Watanzania hapa nchini Italia na kuwaomba wandelee na moyo huo pale panapokuwa na matatizo mengine. Mwenyekiti pia aliwashukuru wanajumuia wote kwa michango yao ya kila mwezi ambayo ndio inafanya jumuiya iwepo pale ilipo sasa. Katibu kwa upande wake aliwashukuru wanajumuiya kwa ujumla kwa ushirikino wao na kuwaomba waendelee na moyo wa kujitoa kwa wengine na kuendelea kuonyesha ushirikiano pale viongozi wanapowatafuta.
Kikao kijacho kitakuwa tarehe29 Machi 2014, kwenye Restaurant ya wahindi maeneo ya Termini. Karibuni sana.
Kikao kijacho kitakuwa tarehe29 Machi 2014, kwenye Restaurant ya wahindi maeneo ya Termini. Karibuni sana.
No comments:
Post a Comment