Siku ya Jumanne, tarehe 19 machi, majira ya saa tatu na nusu asubuhi, Baba Mtakatifu Francis, amezindua rasmi utume na
utawala wake kwa Ibada ya Misa, katika Uwanja wa Kanisa Kuu la
Mtakatifu Petro, mjini Vatican. kwenye Ibada hii ya uzinduzi Baba Mtakatifu ameongoza Ibada pamoja na
Makardinali na Maaskofu wapatao 180 na kuhudhuriwa na Wakuu wa nchi 31,
Viongozi wa Kifalme 6, Wana Wafalme 3, Mawaziri Wakuu 11. Ibada hii iliudhuliwa na umati wa watu, sio tu waumini wa Kikatoliki bali hata waumini wa madhehebu mbalimbali na zaidi tokea dini mbalimbali. Umati wa watu unakadiriwa kutokupungua 200.000.
Katika Ibada hii, Baba Mtakatifu alivalishwa Pete ya Petro na Kardinali Angelo Sodano , ikiwa kama ishara ya wadhifa wake.
Bendera ya Tanzania ilipeperushwa vizuri sana na umati mkubwa wa Watanzania walioudhulia Tukio ili la Kihistoria.
Tunamuombea Baba Mtakatifu Francis, muongozo mwema wa kanisa katoriki kama yeye mwenyewe alivyotuomba.

No comments:
Post a Comment