Mwili wa marehemu Alfonsina ambaye ni dada wa Sr. Blanca Shayo wa Masister wa Ekaristi
Takatifu jana tarehe 14 Febraio 2013 uliagwa na umati wa watu mjini Roma kwenye kanisa la Mtakatifu Dorotea lililopo maeneno ya Trastevere. Marehemu Alfonsina ambaye alikuja nchini Italia tarehe 06.02.2013 kwa dhumuni la kushiriki kwenye sherehe za nadhiri za mdogo wake Sr. Blanca Shayo zilizokuwa zinatarajiwa kufanyika jumamosi
tarehe 09/02/2013 alifariki baada ya kuugua ghafla kesho yake, tarehe 07.02.2013, saa
kumi jioni. Mwili wa marehemu umeondoka leo kuelekea nchini Tanzania kwa Mazishi. Mwenyezi mungu amlaze mahala pema Marehemu Alfonsina. Amen.
NB: Naomba radhi kwa kwa quality ya picha. Picha zilipigwa kwa simu ya mkononi.
No comments:
Post a Comment