Pages

log with Fire

WELCOME TO TANZANIA
Tanzanian Community in Rome, Via GIUSEPPE DI VITTORIO 9, 00067 MORLUPO, Rome, Italy -- Sasa Mnaweza kuweka Michango yenu ya mwezi kwenye account ya Jumuiya: Banki ya Posta:Associazione dei Tanzaniani a Roma Acc. Number 000007564174 Codice Fiscale: 97600810580 ---

welcome to Tanzania

TANZANIAN COMMUNITY IN ROME (TZ-RM,) is a community that unites TANZANIANS living in Rome and those living outside of Rome who have read, understood and accepted the content of its Constitution and hence becoming part of the community's family. Tanzanian Community in Rome is a fruit of the well designed ideas, approved by all community members at the Community's First General Meeting held on the 30th January, 2010. It is a non-political, non-religious, non-ethnical and non-gender based kind of organization. It is a community that democratically, accepts and respects different ideas from all its members without any sort of segregation.

Tanzanian Community in Rome counts alot on members monthly contributions in order to keep the community alive.But all in all, it appreciates any sort of contribution from anyone.

Thursday, May 24, 2012

KUPOKELEWA KWA MWILI WA MAREHEMU PADRE JAMES MBWAMA TANZANIA


                                                      
Taarifa zilizopatikana kutoka Tanzania kupitia mwakilishi wa mapadre wa Mbeya nchini Italia Mh. Padre Kristofa Zulu Nyoni ni kwamba, mwili wa Marehemu Padre JAMES MBWAMA uliwasili salama jijini Dar es salaam, Tanzania tarehe 23/5/2012 muda wa saa 9.30 Alasiri, na kupokelewa na Askofu Gervas Nyaisonga wa Dodoma, Askofu Maluma wa Njombe, na Pd. Magala Vicar General wa Jimbo la Mbeya aliyeambatana na baadhi ya mapadre wa jimbo hilo. Kulikuwa pia na ujumbe wa mapadre wanaofanyakazi katika Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania ambao waliongozwa na Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania. Mh. Padre Makunde. Mama Mkuu wa Shirika la Masista - Jimbo la Mbeya, Mheshimiwa sana Sr. Mirambo aliambatana na Masista kutoka Konventi ya Makoka - Dar es Salaam na Masista wanaofanya kazi Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania. Shughuli hiyo ya kupokea mwili wa mpendwa wetu ilihudhuriwa pia na waamini walei na watu wenye mapenzi mema kutoka kada mbalimbali.

Baada yakupokelewa mwili huo, Askofu Gervas Nyaisonga aliongoza Sala fupi pale pale Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere – Dar es Salaam, na baada ya Sala hiyo na Baraka msafara ulianza safari kuelekea Mbeya kwa mazishi ya Mheshimiwa Padre James Mbwama ambayo yanatarajiwa kufanyika siku ya alhamisi tarehe 24/5/2012.

Wakati huo huo, habari kutoka jimboni Mbeya zinasema, Waamini, Masista na Mapadre wa Jimbo la Mbeya wamefanya Sala maalum ya Mkesha kwa ajili ya kumwombea Marehemu Padre James Mbwama usiku wa kuamkia alhamisi ya tarehe 24/5/2012.

Jimbo la Mbeya linaendelea kutoa shukrani zake za dhati kwa jumuiya nzima ya watanzania Roma kwa ushirikiano waliouonesha tangu pale walipopata taarifa za kuugua ghafla na hatimaye kufariki kwa Padre James Mbwama.

No comments:

Post a Comment