Pages

log with Fire

WELCOME TO TANZANIA
Tanzanian Community in Rome, Via GIUSEPPE DI VITTORIO 9, 00067 MORLUPO, Rome, Italy -- Sasa Mnaweza kuweka Michango yenu ya mwezi kwenye account ya Jumuiya: Banki ya Posta:Associazione dei Tanzaniani a Roma Acc. Number 000007564174 Codice Fiscale: 97600810580 ---

welcome to Tanzania

TANZANIAN COMMUNITY IN ROME (TZ-RM,) is a community that unites TANZANIANS living in Rome and those living outside of Rome who have read, understood and accepted the content of its Constitution and hence becoming part of the community's family. Tanzanian Community in Rome is a fruit of the well designed ideas, approved by all community members at the Community's First General Meeting held on the 30th January, 2010. It is a non-political, non-religious, non-ethnical and non-gender based kind of organization. It is a community that democratically, accepts and respects different ideas from all its members without any sort of segregation.
Tanzanian Community in Rome counts alot on members monthly contributions in order to keep the community alive.But all in all, it appreciates any sort of contribution from anyone.

Tuesday, November 22, 2011

MABADILIKO KWENYE KATIBA

Kwa heshima na taadhima, uongozi wa jumuiya ya Watanzania Rome, unapenda kuwajulisha kuwa, wanajumuiya walioshiriki kwenye mkutano mkuu uliofanyika tarehe 19 Nov. 2011, waliafiki kubadilisha kipengele namba 3.2.4 cha kwenye katiba. mabadiliko haya yataanza kufanya kazi kuanzia tarehe 1 Januari 2012.

Kipengele kilichobadilishwa hapo hawali kilikuwa kinasomeka hivi, "Mchango wa kila mwezi utakuwa ni euro 15, ambazo zinaweza kulipwa kila mwezi au kimafungu ilimradi tu zisicheleweshwe kulipwa zaidi ya miezi mitatu. Wanafunzi wenye miaka chini ya miaka (26) kwenda chini, watapata punguzo la euro 8 na hivyo kutakiwa kulipa euro 7 tu kila mwezi".

Baada ya mabadiliko, kipengele hichi sasa kinasema hivi,"mchango wa kila mwezi utakuwa euro 10 ambazo zinaweza kulipwa kila mwezi au kimafungu ilimradi tu zisicheleweshwe kulipwa zaidi ya miezi mitatu. Wanafunzi wenye miaka chini ya miaka (26) kwenda chini, watapata punguzo la euro 8 na hivyo kutakiwa kulipa euro 7 tu kila mwezi". Wanajumuiya walikubaliana kuwa kipengele hichi kimewekwa kama jaribio kwa kipindi cha mwaka mmoja kuona kama wanajumuiya wataamasika kutochelewesha michango yao ya kila mwezi.

Wanajumuiya kwa pamoja waliafiki pia kuwa, kwa wale wote ambao wanamadeni ya nyuma watatakiwa kuyalipa madeni yao yote kwa kama ilivyokuwa zamani yaani euro 15 kwa kila mwezi.

Andrew Chole Mhella,

Katibu.

No comments:

Post a Comment