Pages

log with Fire

WELCOME TO TANZANIA
Tanzanian Community in Rome, Via GIUSEPPE DI VITTORIO 9, 00067 MORLUPO, Rome, Italy -- Sasa Mnaweza kuweka Michango yenu ya mwezi kwenye account ya Jumuiya: Banki ya Posta:Associazione dei Tanzaniani a Roma Acc. Number 000007564174 Codice Fiscale: 97600810580 ---

welcome to Tanzania

TANZANIAN COMMUNITY IN ROME (TZ-RM,) is a community that unites TANZANIANS living in Rome and those living outside of Rome who have read, understood and accepted the content of its Constitution and hence becoming part of the community's family. Tanzanian Community in Rome is a fruit of the well designed ideas, approved by all community members at the Community's First General Meeting held on the 30th January, 2010. It is a non-political, non-religious, non-ethnical and non-gender based kind of organization. It is a community that democratically, accepts and respects different ideas from all its members without any sort of segregation.

Tanzanian Community in Rome counts alot on members monthly contributions in order to keep the community alive.But all in all, it appreciates any sort of contribution from anyone.

Sunday, May 1, 2011

Rome: Papa Yohane Paulo wa Pili hawa Mwenyeheri



Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita katika mahubiri ya kumtangaza Mtumishi wa Mungu Yohane Paulo wa pili kuwa Mwenyeheri, Mei, Mosi, 2011 anasema, miaka sita iliyopita wakati wa mazishi ya Baba Mtakatifu Yohane Paulo wa pili, watu wengi walijawa na machozi na simanzi kuu, lakini walifarijika kutokana na neema ya Mungu iliyojionesha kwa namna ya pekee katika mji wa Roma na ulimwengu kwa ujumla, kutoka na ushuhuda wa mateso katika hija ya maisha ya mwanadamu; akaonesha pia utakatifu wa maisha.

Kutokana na sababu hizi msingi, kwa kuzingatia sheria na kanuni za Kanisa, mchakato wa kumtangaza Mtumishi wa Mungu Yohane Paulo wa pili kuwa Mwenyeheri umekwenda kwa haraka katika kipindi cha miaka sita tu, tangu alipofariki dunia, kwani ilimpendeza Bwana, Yohane Paulo wa pili kutangazwa kuwa ni Mwenyeheri.

Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, aliwashukuru viongozi wa Kanisa, Serikali, Jumuiya ya Kimataifa, waamini na watu wote wenye mapenzi mema, waliofurika mjini Vaticaan kushuhudia tukio hili la kihistoria, bila kuwasahau wote waliokuwa wamejiunga naye kwa njia ya vyombo vya mawasiliano ya jamii.

Source: Radio Vatican

No comments:

Post a Comment