Pages

log with Fire

WELCOME TO TANZANIA
Tanzanian Community in Rome, Via GIUSEPPE DI VITTORIO 9, 00067 MORLUPO, Rome, Italy -- Sasa Mnaweza kuweka Michango yenu ya mwezi kwenye account ya Jumuiya: Banki ya Posta:Associazione dei Tanzaniani a Roma Acc. Number 000007564174 Codice Fiscale: 97600810580 ---

welcome to Tanzania

TANZANIAN COMMUNITY IN ROME (TZ-RM,) is a community that unites TANZANIANS living in Rome and those living outside of Rome who have read, understood and accepted the content of its Constitution and hence becoming part of the community's family. Tanzanian Community in Rome is a fruit of the well designed ideas, approved by all community members at the Community's First General Meeting held on the 30th January, 2010. It is a non-political, non-religious, non-ethnical and non-gender based kind of organization. It is a community that democratically, accepts and respects different ideas from all its members without any sort of segregation.
Tanzanian Community in Rome counts alot on members monthly contributions in order to keep the community alive.But all in all, it appreciates any sort of contribution from anyone.

Friday, May 13, 2011

MWALIKO KUTOKA CHAMA CHA WANAFUNZI WAKATORIKI WATANZANIA ROMA

Jumuiya ya Watanzania Roma
Tunapenda kuwashukuru kwa mwaliko wa kushiriki kwenye sherehe ya muungano wa Tanzania. Tumezingatia mabadiliko ya tarehe. Tunawahakikishia uwepo wa uwakilishi wetu katika sku hiyo.

Aidha tunapenda pia kuwaalika katika Kikao chetu cha mwaka keshokutwa Jumapili 15.04.2011, kitakachokuwa na malengo matatu:- 1.Kuuenzi muungano wa Taifa letu la Tanzania kama ilivyo kawaida yetu. 2. Kumshukuru Mungu kwa kupata mashemasi wapya, Celestine Nyanda na Patience Nahondi. 3. Kuwaombea na kuwaaga wanafunzi wanaomaliza masomo yao. Kikao hiki kitaanza saa 4:00 asubuhi na kitafanyikia kwa Wamissionari wa Bikira Maria wa La Salette, katika nyumba yao kuu inapatikana Piazza Madonna della salette, 3.

NAMNA YA KUFIKA:-
Kwa wanaotoka maeneo ya Cornelia wachukue basi namba 791 watelemke kituo kinaitwa San Giovanni di Dio, Piazza san Giovanni di Dio. Ukiwa kwenye Piazza ukiangalia mbele yako utaona mnara wa kanisa. Uje hapo utapokelewa.

Kwa wanaotoka maeneo ya Stazione Termini wachukue basi namba H watelemke kituo kinaitwa San Giovanni di Dio, Piazza san Giovanni di Dio. Ukiwa kwenye Piazza ukiangalia mbele yako utaona mnara wa kanisa. Uje hapo utapokelewa.

Kwa wanaotoka maeneo ya Laterani wachukue basi namba 3 watelemke Stazione Trastevere kisha wachukue tram namba 8 watelemke kituo kinaitwa San Giovanni di Dio, Piazza san Giovanni di Dio. Ukiwa kwenye Piazza ukiangalia mbele yako utaona mnara wa kanisa. Uje hapo utapokelewa.

Kwa wanaotoka maeneo ya largo Argentina wachukue basi tram namba 8 watelemke kituo kinaitwa San Giovanni di Dio, piazza san Giovanni di Dio. Ukiwa kwenye Piazza ukiangalia mbele yako utaona mnara wa kanisa. Uje hapo utapokelewa.

Kwa wanaotoka maeneo ya Vatican wachukue kutoka kituo cha mabasi cha Hospitali ya Santo Spirito basi namba 870 watelemke kituo kinaitwa Zambareli. Warudi nyuma mita 10 na kufuata barabara iliyo kulia kwao mpaka mwisho ukiangalia mbele yako utaona mnara wa kanisa la Parokia della Madonna della Salette. Uje hapo utapokelewa.

Pamoja na mazingira ya kuchelewa kuwaalika, ambayo tunaomba mtukalie radhi, tunasema Karibuni sana.

Padre Emmanuel Nyaumba

katibu

No comments:

Post a Comment