Pages

log with Fire

WELCOME TO TANZANIA
Tanzanian Community in Rome, Via GIUSEPPE DI VITTORIO 9, 00067 MORLUPO, Rome, Italy -- Sasa Mnaweza kuweka Michango yenu ya mwezi kwenye account ya Jumuiya: Banki ya Posta:Associazione dei Tanzaniani a Roma Acc. Number 000007564174 Codice Fiscale: 97600810580 ---

welcome to Tanzania

TANZANIAN COMMUNITY IN ROME (TZ-RM,) is a community that unites TANZANIANS living in Rome and those living outside of Rome who have read, understood and accepted the content of its Constitution and hence becoming part of the community's family. Tanzanian Community in Rome is a fruit of the well designed ideas, approved by all community members at the Community's First General Meeting held on the 30th January, 2010. It is a non-political, non-religious, non-ethnical and non-gender based kind of organization. It is a community that democratically, accepts and respects different ideas from all its members without any sort of segregation.

Tanzanian Community in Rome counts alot on members monthly contributions in order to keep the community alive.But all in all, it appreciates any sort of contribution from anyone.

Thursday, December 16, 2010

PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI YA JUMUIYA 2010

Tunakaribia kuumaliza Mwaka 2010 nakuukaribisha mwaka 2011. Kwa Jumuiya ya Watanzania Rome, mwaka huu hautasahaulika hata simu moja kwenye historia ya Jumuiya yetu maana ni mwaka ambao Jumuiya yetu ilianzishwa na kuweza kupata mafanikio mengi sana kadri siku zinavyozidi kwenda. Hapo chini kunapicha za matukio mbalimbali yaliyotokea kuanzia tarehe 30 January mpaka Disemba 2010.

1.Mkutano wa ufunguzi wa Jumuiya ya Watanzania Rome 30 Januari
2010
Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Rome Ndugu Andrew Chole Mhella, akisema mawili matatu kabla ya kumkaribisha Mh. Andrew Kyabashasa kuongoza kikao na Kumkaribisha pia Mgeni rasmi ambaye alikuwa Msimamizi mkuu, Kaimu Balozi Mh.Mbilinyi.

Wajumbe waliokuwepo walimchagua Mh. Andrew Kyabashasa ( katikati) kuwa mwenyekiti wa muda ili aweze kuongoza kikao ambacho kwanza kilianza kwa kujadili na kupitisha katiba na baadae uchaguzi wa viongozi. Mkutano ulikuwa chini ya usimamizi wa kaimu Balozi Mh. Mbilinyi kulia na kushoto ni Katibu wa Jumuiya, ndugu Andrew Chole Mhella.

Watanzania waliofika kushiriki kwenye huu mkutano walitoka sehemu mbalimbali za Rome. Pichani, mwenye tie ni ndugu Leonce Uwandameno ambaye baadae alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa jumuiya akisikiliza kwa umakini majadiliano ya katiba. Kushoto kabisa ni Bi.Diana ambaye alichaguliwa kuwa Katibu Msaidizi na anayemfuatia ni Bi. Zainab na kulia ni bi. Khadija Mjumbe wa Jumuiya.

Viongozi wapya wakiwasalimia Watanzania waliokuwepo baada ya kuchaguliwa kuiongoza Jumuiya. Kutoka Kushoto ni ndugu Andrew Chole Mhella(Katibu), Mh. Erasmus Pindu Luhoyo(Mwenyekiti Msaidizi), katikati ni Mh.Leonce Uwandameno(Mwenyekiti), ndugu Awadhi Suleiman(Mweka Hazina) na Bi. Diana Paul Olotu(Katibu Msaidizi).



2.Sherehe ya Muungano 2010
Kwa juu ni picha ya Mama Balozi pamoja na wakina mama wakitanzania.


Hapa pembeni ni Viongozi wa Jumuiya pamoja na Mgeni Rasmi, Balozi wa Tanzania nchi Italy, Mheshimiwa Abeid Amani Karume pamoja na Mama Balozi.



Wengi walijumuika kusherekea Muungano wa Tanzania.










3.Mkutano Mkuu wam Kufunga Mwaka wa Jumuiya ya Watanzania Rome 27 Nov. 2010

Wanajumuiya pamoja na Kaimu Balozi Mheshimiwa Salvatory Mbilinyi baada ya Mkutano






Mwaka wa Jumuiya Ulifungwa namna Hii kama mnavyoona!
Good Luck ndugu Zanguni Watanzania!!!!Mambo Matamu Uongozi unawaandalia kwenye Mwaka Mpya 2011!!

No comments:

Post a Comment