Pages

log with Fire

WELCOME TO TANZANIA
Tanzanian Community in Rome, Via GIUSEPPE DI VITTORIO 9, 00067 MORLUPO, Rome, Italy -- Sasa Mnaweza kuweka Michango yenu ya mwezi kwenye account ya Jumuiya: Banki ya Posta:Associazione dei Tanzaniani a Roma Acc. Number 000007564174 Codice Fiscale: 97600810580 ---

welcome to Tanzania

TANZANIAN COMMUNITY IN ROME (TZ-RM,) is a community that unites TANZANIANS living in Rome and those living outside of Rome who have read, understood and accepted the content of its Constitution and hence becoming part of the community's family. Tanzanian Community in Rome is a fruit of the well designed ideas, approved by all community members at the Community's First General Meeting held on the 30th January, 2010. It is a non-political, non-religious, non-ethnical and non-gender based kind of organization. It is a community that democratically, accepts and respects different ideas from all its members without any sort of segregation.

Tanzanian Community in Rome counts alot on members monthly contributions in order to keep the community alive.But all in all, it appreciates any sort of contribution from anyone.

Sunday, November 28, 2010

Rome: Mkutano Mkuu wa Kwanza wa kufunga Mwaka wa Jumuiya ya Watanzania Rome (TZ-RM) Wafana


Pichani ni Mheshimiwa Salvator Mbilinyi akitoa speech, Waliokaa ni Viongozi wa Jumuiya ya Watanzania Rome. Kutoka kushoto ni ndg. Awadh Suleiman(Mweka Hazina), anafuata Mwenyekiti wa Watanzania Rome, Mh. Leonce Uwandameno na wa Mwisho kulia ni Katibu wa Jumuiya ndugu Andrew Chole Mhella.

Rome: Mkutano mkuu wa kwanza wa kufunga mwaka wa Jumuiya ya Watanzania Rome,ulifanyika jana(27 Nov. 2010) na kuleta mafanikio mengi.Mkutano huu ambao ulihudhuriwa si tu na Watanzania watokao Rome bali na baadhi waliotoka nje ya Rome kama vile, ndugu Mwinyimwaka ambaye ni mmoja wa viongozi wa watanzania mjini modena. Mgeni rasmi kwenye mkutano huu alikuwa ni Naibu Balozi wa ubalozi wa Tanzania nchini Italy, Mh.Salvator Mbilinyi. Kwenye mkutano huu Jumuiya pia ilipata ugeni wa Mfanyabiasha raia wa Kitaliano aliyekuja kuelezea nia yake za kuanzisha biashara nchini Tanzania pamoja na mkurugenzi wa BANCA ETICA DIASPORA AFRICANA Dr.Francis pamoja na makamu wake ndugu Cheikh Tidiane Khoumanza waliokuja kuelezea namna gani banki waliyoanzisha inafanya kazi na kushawishi watanzania kujiunga na Bank hii.

Mwenyekiti alifungua kikao kwa Kuushukuru ubalozi wa Tanzania chini Italy na wafanyakazi wake wote waliosaidia kwa mamna moja au nyingine kufanikisha shughuli nzima na zaidi kwa kutupatia nafasi kufanya mkutano kwenye Ubalozi. Mwenyekiti pia alimshukuru mgeni rasmi kwa kukubali mwaliko wa kujumuika na Wanajumuiya kwenye mkutano huu, pamoja na watanzania wote na wageni wote waliofika kwenye mkutano huo muhimu kwa Jumuiya.

Mwenyekiti alielezea mafanikio makubwa ambayo jumuiya iliyapata kwa kipindi cha Mwaka mmoja kama vile:
-Kuongezeka kwa Wanajumuiya siku hadi siku. Wanajumuiya ambao wameomba kujiunga na jumuiya si tu wa Rome, bali hata wengine wanaotoka nje ya Rome.
-Alielezea pia mafanikio yameonekana pia kwenye juhudi za utoaji michango zilizoonyeshwa na Wanajumuia zinaridhisha na kuwaomba wanajumuiya waendelee na moyo huo huo maana jumuiya si jumuiya ya kufa na kuzikana tu bali, inamipango mingi ya maendeleo.
-Jumuiya pia, alieleza mwenyekiti pia imefanikiwa kusajiliwa na taasisi husika ya serikali ya Italia na kufanikiwa tulikabidhiwa hati “CERTIFICATO DI ATTRIBUZIONE DEL CODICE FISCALE 9760081058” na pia kuandikishwa kwenye “AGENZIE DELLE ENTRATE DIREZIONE PROVINCIALE I di ROMA, ufficio Territoriale di Roma 2 Aurelio, kwa No. 6301,serie 3”,siku ya 08/06/2010). Kwa upande wa kujisajili katika serikali yetu ya
Tanzania kupitia Ubalozi wa Tanzania Italy, Mwenyekiti alieleza kuwa Jumuiya iko mbioni kukamilisha kipengele cha mwisho cha kutafsiri kwa lugha ya kiswahili hati zilizo kwenye lugha ya kitaliano.
-Kwenye ushirikiano na Jumuiya nyingine za watanzania, mwenyekiti alieleza kuwa,jumuiya ya watanzania Roma imeendeleza tunu ya watanzania ya umoja na mshikamano na wakitanzania wenzetu Roma na Italia kwa ujumla. Katika kipindi hiki cha mwaka mmoja Jumuiya imekuwa karibu sana Umoja wa Wanafunzi Watanzania Wakatoliki Roma. Aidha Jumuiya imekuwa ikituma mialiko ya kukaa pamoja na kujadiliana na uongozi wa jumuiya mbali mbali za kitanzania ila uongozi wa jumuiya moja ndio kwa sababu zake binafsi haijaonesha nia ya ushirikiano huu. Jumuiya ya Watanzania Rome, aliendelea Mh.Mwenyekiti kwa kuushukuru uongozi wa Watanzania Modena kwa kuonyesha ushirikiano mzuri kwenye maswala mbalimbali,kwani jumuiya yetu bado inaamini kuwa Umoja ni nguvu na Utengano ni Udhaifu.
Kwenye mkutano huu, mgeni Rasmi, Mh. Salvator Mbilinyi, Naibu Balozi wa ubalozi wa Tanzania Italy, aliwashukuru sana Viongozi na wanajumuiya yake kwa kumwalika kwenye mkutano mkuu wa Kwanza wa kufunga mwaka wa Jumuiya ya Watanzania Rome. Mh Mbilinyi alielezea kufarijika kuona jumuiya ikishirikiana kwa hali na mali kufanikisha maswala kadhaa. Mheshimiwa pia aliahidi kutembelea jumuiya mbalimbali za kitanzania zilizopo nchini Italy ili kuweza kuona uwezekano wa kuanzisha kwa PAMOJA jumuiya moja itakayo waunganisha Watanzania. Jumuiya ambayo itawashirikisha watanzania wote kutoka sehemu mbalimbali za Italia na ambayo kwa pamoja itaundwa kulingana na matakwa ya wanajumuiya wake wote na si kwa madhumuni binafsi na kisha kuitisha uchaguzi utakao jumuisha watanzania kutoka sehemu mbalimbali nchini Italy kwa pamoja.
Kwenye mkutano huu Jumuiya pia iliweza kumuaga Moja wa mwanajumnuiya mwanzilishi ambaye ameamishwa kikazi. Kwa niaba ya Wanajumuiya wote tunamtakia maisha mema huko aendako.

Mwisho kabisa, Jumuiya ya Watanzania Rome, inapenda kutoa shukrani kwa Ubalozi wa Tanzania nchini Italy kwa ushirikiano mkubwa waliouonyesha kwenye kufanikisha mkutano huu.

Mungu ibariki Tanzania na watu wake.



Bwana fedha akielezea mwenendo wa Fedha.




Mambo hayakuwa mabaya..ni maandalizi ya Moto wa Nyama Choma.


MSOSI NDIO KAMA MNAVYONA WENYEWE!




Wanajumuiya wakiselebuka!!


Mjumbe Khadija mwenye browse nyekundu alikuwepo pia!

Cheers ya Kumuaga Mjumbe Andrew Kybashasa




Flowers walijuwepo pia.

2 comments:

  1. Du!!! Tunawaoneeni husuda.. yaani mmejitahidi kuendeleza jumuiya kwa misingi hasa ya jumuiya siyo ya ubabaishaji! Wenzenu hapa modena ni fujo tu! haijulikani katiba ipi tunafuata na jumuiya ipi na tunafuata nini au nani. Yaani tumekuwa bendera fata upepo na tumeshindwa kusimama na miguu yetu wenyewe kama wenzetu. Yaani tunaburuzwa tu kwa sana na wenzetu wa gomora!! kila wanachosema sisi yetu ndiyo tu ndiyo maana hatuna umoja unaoeleweka... kweli natamani kujiunga na umoja wenu, Roma... nifanyeje? Tumechoka na ubabaishaji!!! watu wengi hapa wanataka tujitegemee wenyewe na tufanye mambo yetu wenyewe... mbona watanzania tuko wengi tu hapa Modena na Bologna, nini kinashindikana?
    Hongera sana..wenzetu wa Roma.

    Mtemahanji, Bologna

    ReplyDelete
  2. Ndugu yangu mtemahanji, habari za leo. Asante sana kwa kufuatilia blog yetu na tunafurahi kwa pongezi ulizotupatia. Tutafute kwa e-mail hii (watanzaniaroma@yahoo.it) tutaongea mengi zaidi yanayohusu jumuiya yetu.Na tutawashauri nini cha kufanya ili muweze kuimarisha jumuiya yenu.Sisi tunaamini chochote kinawezekana panapokuwa na nia. Asante

    ReplyDelete