Ni muhimu kukumbushana kuwa, Jumuiya ya Watanzania Rome ni jumuiya ambayo si ya KISIASA, Kidini wala kikabila. Ni Jumuiya iliyoanzishwa na WATANZANIA waishio Rome na wachache waishio nje ya Rome, ambao kwa PAMOJA waliamua kutengeneza KATIBA ambayo ndio usukani wa jumuiya. Jumuiya ya Watanzania Roma ni jumuiya iliyoundwa ili kuondoa kiu cha Watanzania wengi ambao walikuwa hawajapata chombo cha kuwasikiliza na zaidi chombo ambacho kiliwapa nafasi ya kuchangia mawazo yao kwenye utengenezaji wa Katiba. Kwa mantiki hiyo basi, Katiba ya jumuiya ya Watanzania Rome imetengezwa na kupigiwa kura na kisha kupitishwa na WATANZANIA siku ya 30 Januari 2010. Ili kuweza kuimarisha umoja wetu mnaombwa mfike kwa wingi maana mawazo yenu ndio yanayofanikisha malengo ya Jumuiya yetu. Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ubariki umoja wa Jumuiya ya Watanzania Roma.
Hapa ndivyo panavyoonekana kwa nje. Kwa ndani kunakaukumbi.
Picha imepigwa na ndugu George Mayaka.
Katibu,
Andrew Chole Mhella
No comments:
Post a Comment