
Timu ya Inter Milan muda si mrefu, yaani leo jioni wamechukua ubingwa wa mpira wa miguu hapa nchini Italia kwa mara ya tano mfululizo. Inter ambayo ilikuwa inaongoza kwa pointi mbili zidi ya Roma mpaka kipindi cha kwanza ilikuwa ikitoa draw na siena kitu ambacho kiliwatia wasiwasi mashabiki wake kutokana na Rome kuwa wanaongoza zidi ya Chievo na hivyo kuwa wao ndio walikuwa wachukue ubingwa. Kipindi cha pili Diego milito aliipatia inter goli la ushindi ambalo ndio lilitowapa inter ubingwa wa hapa nchini Italia.
No comments:
Post a Comment