Pages

log with Fire

WELCOME TO TANZANIA
Tanzanian Community in Rome, Via GIUSEPPE DI VITTORIO 9, 00067 MORLUPO, Rome, Italy -- Sasa Mnaweza kuweka Michango yenu ya mwezi kwenye account ya Jumuiya: Banki ya Posta:Associazione dei Tanzaniani a Roma Acc. Number 000007564174 Codice Fiscale: 97600810580 ---

welcome to Tanzania

TANZANIAN COMMUNITY IN ROME (TZ-RM,) is a community that unites TANZANIANS living in Rome and those living outside of Rome who have read, understood and accepted the content of its Constitution and hence becoming part of the community's family. Tanzanian Community in Rome is a fruit of the well designed ideas, approved by all community members at the Community's First General Meeting held on the 30th January, 2010. It is a non-political, non-religious, non-ethnical and non-gender based kind of organization. It is a community that democratically, accepts and respects different ideas from all its members without any sort of segregation.

Tanzanian Community in Rome counts alot on members monthly contributions in order to keep the community alive.But all in all, it appreciates any sort of contribution from anyone.

Sunday, April 25, 2010

Rome: Watanzania Wengi wajitokeza kusherekea Sherehe ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania



Picha kabla ya Sherehe kuanza




Mheshimiwa Balozi akiwasili ukumbini.


Mama Balozi akiingia ukumbini.


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Roma, Mh. Leonce P. Uwandameno, akimkaribisha mgeni wa rasmi.


Mh. Balozi na Mama Balozi wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Roma.



Picha ya Pamoja (Viongozi wa Jumuiya ya Watanzania Roma na Mh. Balozi na Mama Balozi)

Rome: Jana Jioni Watanzania wengi walijitokeza kusherekea sikukuu ya kuadhimisha miaka 46 ya muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sherehe ambayo ilibidi ifanyike siku ya kesho jumatatu tarehe 26 April, ilifanyika jumamosi tarehe 24 ili kuwezesha hata watanzania wanaokaa nje ya Roma kushiriki. Mgeni rasmi alikuwa Mh.balozi Ali Abeid Aman Karume. Alipokuwa anaongea na Watanzania, Mheshimiwa Balozi, alielezea Umuhimu wa muungano ambao uliletwa kwa jitiada za Hayati Mwalimu Julius Kambarage nyerere na hayati Rais wa Zanzibar wa kipindi hicho Mh. Abeid Aman Karume.

Ifuatayo ni speech ya Mh. mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Roma, ndugu Leonce P. Uwandameno:

-Mheshimiwa Balozi,
-Waheshimiwa Maafisa wa Ubalozi,
-Waheshimiwa wafanyakazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa Roma, FAO na
WFP,
wanajumuiya wenzangu wa Jumuiya ya Watanzania Roma,
*watanzania ambao mpo hapa.
*mabibi na mabwana.

Kwa niaba ya Wanajumuiya ya watanzania Roma, ningependa kuwakaribisheni wote kwenye ukumbi huu ili kwa pamoja tuweze kusherehekea sikukuu ya Muungano.

Kabla sijakukaribisha mgeni rasmi, mheshimiwa Balozi ili uweze kutueleza Umuhimu wa Muungano kwa taifa letu leo hii na kutupa machache juu ya hali ya halisi ya nyumbani ulikokuwa hadi wiki chache zilizoipita, ningependa kuwakumbusheni watanzania wenzangu mambo machache juu ya Shereh hii ya leo.

Mheshimiwa balozi, kutokana na tarehe ya Muungano ambayo ni tarehe 26 .04 kuangukia siku ya Jumatatu, ambapo kwa hali ilivyo hapa ugenini imeonekana ni vigumu kuweza kukusanyika watanzania wengi kwa pamoja ili tuweze kusherehekea muungano. Hii ndiyo sababu iliyotufanya tuamue kusherehekea leo hii tarehe 24 Aprili. Hata hivyo ningenda kuwakumbusha watanzania wenzangu hasa vijana au watoto waliozaliwa miaka ya hivi karibuni kuwa Tanganyika na Zanzibar tarehe 26.4.1964 ziliungana na kuunda jina la nchi yetu kuwa Tanzania.

Mheshimiwa Balozi, ningependa pia kuwakumbusha Watanzania wenzagu kuwa katika miaka ya 1960 zilikuwepo jitihada nyingi za kuunganisha nchi za Kiafrika ili kurudisha umoja, undugu na mshikamano wa kiAfrika ulivunjwa kwa hila na mipaka ya wakoloni. Lakini jitihada hizo zote zilishindwa kufikiwa, isipokuwa Muungano wetu tu. Yaani ni sisi Watanganyika na Wanzibar ndiyo tulioweza. Na siyo tu kuweza kufikia Muungano bali hata kuudumisha. Historia ya Afrika inatukumbusha kwamba nchi ya Senegal na Gambia pia ziliungana katika kipindi fulani , lakini Muungano wao haukudumu, ulisarambatika upesi sana. Lakini Muungano wetu umefikisha miaka 46, na bado upo imara. Hivyo tuna kila sababu ya kujivunia.

Yote hii ni kwa sababu nguvu ya Muungano wetu ni sisi Watanzania wenyewe, na ndiyo sababu inayotupa furaha hata sisi watanzania hapa Roma ya kukusanyika jioni hii ili kushehekea muungano wetu, kwa kupokea nasaha zako Mheshimiwa Balozi, huku tukila, tukinywa.

Mwisho kabisa Mheshimiwa Balozi ningependa kwa namna ya Pekee kwa pamoja tuwakumbuke mababa wawili wa Taifa letu ambao ndio waasisi wa muungano wetu. Hawa ni Mzee Sheikh Abeid Amani Karume kwa Upande wa Zanzibari na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa upande wa Tanzanyika ambao kwa upendo mpana sana na ujasiri mkubwa sana waliweza kufanya maamuzi muhimu sana ya kisiasa hasa ya kutimiza ndoto za wanzibari na watanganyika ya kuungana tena baada ya kutenganishwa na wakoloni.

Mungu Ibariki Tanzania.
Mungu Abariki Muungano wetu.

Mwenyekiti wa Jumuiya wa Watanzania, Roma.
Leonce Protas Uwandameno.

No comments:

Post a Comment