
Jumuiya ya Watanzania Roma inaungana na Watanzania wengine duniani kuomboleza kifo cha balozi Daudi Mwakawago kilichotokea leo kwenye hospitali ya Aga Khan mjini Dar-es-Salaam, Tanzania. Marehemu Daudi Mwakawago atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa alioutoa kwenye maendeleo ya nchi yetu. Marehemu Mwakawago kabla ya kustahafu alishika nyadhifa mbalimbali serikalini, pamoja na kuwa balozi wetu wa Tanzania hapa nchini Italia kwenye miaka ya tisini mwanzoni. Kwa kipindi alichokuwa hapa Rome, marehemu Mwakawago alikuwa karibu sana na watanzania na zaidi alikuwa anapenda sana uwepo wa jumuiya ambazo sasa zipo. Mwenyezi Mungu aipe nguvu familia ya marehemu Mwakawago kwenye kipindi hiki kigumu. MWENYEZI MUNGU AMPUMZISHE KWA AMANI MAREHEMU DAUDI MWAKAWAGO, AMEN.
Rest in peace mzee wetu Mwakawago!!
ReplyDelete