Pages

log with Fire

WELCOME TO TANZANIA
Tanzanian Community in Rome, Via GIUSEPPE DI VITTORIO 9, 00067 MORLUPO, Rome, Italy -- Sasa Mnaweza kuweka Michango yenu ya mwezi kwenye account ya Jumuiya: Banki ya Posta:Associazione dei Tanzaniani a Roma Acc. Number 000007564174 Codice Fiscale: 97600810580 ---

welcome to Tanzania

TANZANIAN COMMUNITY IN ROME (TZ-RM,) is a community that unites TANZANIANS living in Rome and those living outside of Rome who have read, understood and accepted the content of its Constitution and hence becoming part of the community's family. Tanzanian Community in Rome is a fruit of the well designed ideas, approved by all community members at the Community's First General Meeting held on the 30th January, 2010. It is a non-political, non-religious, non-ethnical and non-gender based kind of organization. It is a community that democratically, accepts and respects different ideas from all its members without any sort of segregation.
Tanzanian Community in Rome counts alot on members monthly contributions in order to keep the community alive.But all in all, it appreciates any sort of contribution from anyone.

Thursday, January 7, 2010

Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Watanzania Roma

Kwa Heshima na taadhima kutoka kwenye uongozi wa Jumuiya ya Watanzania Rome, ninayo furaha ya kuwajulisha watanzania wote muishio Rome kuwa siku ya tarehe 30 January 2010, tutakuwa na mkutano mkuu wa Jumuiya ya Watanzania Rome. Mkutano huu utakuwa na malengo makuu mawili:
Kwanza kabisa mkutano utalenga kupitisha katiba mpya ya Jumuiya ya watanzania Rome. Kuanzia leo pendekezo la katiba yaani proposal kwa lugha ya kiingeleza, imeanza kusambazwa kwa watanzania mbalimbali hapa Rome kwaajiri ya kutoa maoni na mapendekezo yao yenye lengo la kuimarisha na kuboresha hii katiba na Jumuiya yetu kwa ujumla. Hii yote imetokana na maombi mengi tuliyoyapata kutoka kwa watanzania mbalimbali.
Pili ni kutakuwa na zoezi la kumchagua mwenyekiti mpya wa Jumuiya hii ya Rome na wajumbe wapya watakao ongoza Jumuiya yetu kwa kipindi kitakachopitishwa kwenye katiba yetu.

Kwa wale ambao hawajapata pendekezo la Katiba mnaombwa mniandikie e-mail na mimi haraka iwezekanavyo ntawatumieni.

Ili kufanikisha mkutano huu na shughuli nzima ya mkutano, tunaomba mchango wenu wa euro 15 ikiwezekana kabla ya tarehe 23 January. Mchango huu mnaweza kuwakilisha moja kwa moja kwa mweka hazina wa jumuiya Ndg. Awadhi. Mnaweza kumpata kwa namba hii ya simu 3395438783 au ndugu Mayaka kwa namba hii 3484617229. Kwa maelezo zaidi ya shughuli nzima unaweza kumwandikia Katibu kwenye e-mail hii watanzaniaroma@yahoo.com.

Ukumbi upo kwenye mtaa ule ule ambao tunafanyiaga mikutano yetu, Via Cassalattico 6 maeneo ya Via cassia - Grottarossa. Tutawajulisha muda na programme nzima mapema iwezekanavyo.

Kwaniaba ya Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania Roma, nawashukuru sana kwa msaada wenu.

Andrew Chole Mhella
Katibu

No comments:

Post a Comment