
Waziri mkuu wa Italia, Mh. Berlusconi, leo tarehe 17 Disemba, ameruhusiwa kutoka hospitali ambapo alikuwa akitibiwa majeraha aliyoyapata baada ya kushambuliwa kwa kurushiwa kasanamu jumapili iliyopita. Berlusconi ambaye alitegemewa kuruhusiwa jana lakini kutokana na hali yake alishauriwa kubakia mpaka leo. Berlusconi ameshauliwa kupumzika kwa siku kumi na tano bila kujishughulisha na shughuli zozote za kijamii au kisiasa.
No comments:
Post a Comment