
Confederation Cup ni kombe linalo jumuisha mabingwa kwa mabala yote Duniani wakiongezwa pia washindi wa Kombe la Dunia na mwenyeji wa michezio kama ambavyo ilivyo sasa kwa Sauzi Africa. Kwa mwaka huu kombe limeweza kutupatia burudani nzuri sana ambapo tumeweza kuona mechi zikichezwa kwa kiwango cha juu sana na kuona timu zikiwa na ushindani mkali sana. Mfano mzuri ni kama Timu za Africa (Sauzi Africa na Egypt), wanavyoendelea kufanya vizuri. Wenyeji wameweza kucheza gemu mbili nzuri mpaka sasa, ambapo mechi ya Kwanza wameweza kutoka sale na Iraq bila bila, na mechi ya pili wameweza kuiliza Timu ya New Zealand kwa Mabao mawili kwa bila. Timu ya Egypt imeweza kuwabuluza mabingwa wa Dunia-Italia- kwa Bao moja bila. Ambapo Italia inatakiwa kuwafunga Brazil kwa mabao mawili ya zaidi ili iweze kusonga, ambayo mpaka sasa kwenye Kombe hili aijapotesa hata point moja ili iweze kusonga mbele ikiombea Wa Egypt wafungwe. Tuombee timu zetu za Africa ziweze kufika mbali hata kwenye Fainali. ukitaka kupata habari zaidi kuhusu Kombe ili tembelea mtandao huu http://www.fifa.com/confederationscup/index.html.
No comments:
Post a Comment