Mkutano wa Watanzania waishio Roma uliofanyika tarehe 29 September 2019 kwenye ukumbi wa ubalozi wa Tanzania nchini Italy ulikuwa na mafanikio sana. Mkutano huu ambao uliandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Italy, chini ya balozi Watanzania nchin Italia, Mh. George Kahema Madafa pamoja na Jumuiya ya Watanzania Roma, ulikuwa na agenda kuu mbili; ya kwanza, ni kuchagua viongozi wapya, baada ya muda wao kuisha; pili kusikiliza ujumbe wa serikali kutoka kwa Mh. Balozi juu ya maswala mbalimbali ambayo yanatugusa sisi Watanzania tuishio ughaubuni.
Kwenye Mkutano huu, viongozi waliochaguliwa ni hawa wafuatao;
1. Leonce Uwandameno (Mwenyekiti)
2. Anastasia Lubangula (Katibu)
3. Irene Mutungi Kaigarula (Mweka Hazina)
Wajumbe wa Kamati kuu waliochaguliwa ni:
1. Andrew Chole Mhella
2. Mwishehe Abeid
3. Pendo
Picha zote zimeletwa kwa isani ya Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti Mstaaafu,
Ndugu Andrew Chole Mhella.
No comments:
Post a Comment