Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Italy kupitia Jumuiya ya Watanzania Roma, unapenda kuwafahamisha kuwa, Wizara ya Mambo ya Nje kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais na Utawala Bora — Zanzibar na Ofisi ya Waziri Mkuu zinaandaa Kongamano la Diaspora (Diaspora Investment Conference) litakalofanyika katika hoteli ya Serena, Dar es Salaam tarehe 13 — 15 Agosti 2015. Aidha imependekezwa kwamba tarehe 15 Agosti 2015
Diaspora watafanya ziara ya kwenda Zanzibar kwa mwaliko wa Serikali ya Zanzibar.
Kongamano hili litafunguliwa na Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na litafungwa na Mhe. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Kongamano la mwaka huu lina kaulimbiu "Creating linkages between Diaspora and Local SMEs in Tanzania" na litajikita katika kuhamasisha ushiriki wa Diaspora katika kukuza biashara ndogo na kati. Aidha kongamano hili pia litahusisha Mikoa ya Tanzania ambapo watapata nafasi ya kunadi fursa za uwekezaji zilizopo Mikoani.
Matukio muhimu yatakuwa ni maonesho ya kibiashara, mada na majadiliano kuhusu ushirikishwaji wa Diaspora kwa maendeleo ya nchi hususan SMEs, uwekezaji mikoani nk.
Tafadhali upatapo ujumbe huu mfahamishe na mwenzako maana kongamano hili ni muhimu kwa Watanzania wote wishio nje ya nchi. Ghalama zote ni za mshiriki.
No comments:
Post a Comment