Mheshimiwa Balozi katikati pamoja na Mh. Mwinyimwaka upande wa kulia. |
Balozi wa Tanzania nchini Italy, Mh. James Msekela, mwishoni mwa wiki iliyopita, alifanya ziara mjini modena. Modena, mji ambao upo kaskazini mwa Italia, ni mji ambao unasifika sana kwa kuwa na viwanda vingi nhapa chini Italia.
Mheshmiwa balozi aliyepokelewa na mwenyeji wake ambaye ni Katibu wa Watanzania Modena, Mh. Mwinyimwaka. Mheshimwa balozi aliwasili mjini modena ijumaa ya tarehe 20 Julai na siku hiyo hiyo mchana, aliweza kutembelea kiwanda cha uzalisha vigae, kilichopo kwenye kitongoji cha Sassuolo, mjini modena.
Siku ya Jumamos, tarehe 21 Julai, Mheshiwa balozi alikutana na Mayor wa CASTELFRANCO, Mh. Stefano Reggianini ambapo walizungumza maswala mbalimbali kuhusiana nauzalishaji na uwekezaji nchini Tanzania.
Baada ya kukutana na Mayor wa Castelfranco, Mheshiwa balozi aliweza kukutana na watanzania kwenye ukumbi wa ex-bliblioteca ambapo pamoja na Watanzania walijadili maswali mbalimbali.
Habari na picha zimeletwa kwetu na Mh. Mwinyimwaka, Katibu wa Watanzania Modena.
No comments:
Post a Comment