Pages

log with Fire

WELCOME TO TANZANIA
Tanzanian Community in Rome, Via GIUSEPPE DI VITTORIO 9, 00067 MORLUPO, Rome, Italy -- Sasa Mnaweza kuweka Michango yenu ya mwezi kwenye account ya Jumuiya: Banki ya Posta:Associazione dei Tanzaniani a Roma Acc. Number 000007564174 Codice Fiscale: 97600810580 ---

welcome to Tanzania

TANZANIAN COMMUNITY IN ROME (TZ-RM,) is a community that unites TANZANIANS living in Rome and those living outside of Rome who have read, understood and accepted the content of its Constitution and hence becoming part of the community's family. Tanzanian Community in Rome is a fruit of the well designed ideas, approved by all community members at the Community's First General Meeting held on the 30th January, 2010. It is a non-political, non-religious, non-ethnical and non-gender based kind of organization. It is a community that democratically, accepts and respects different ideas from all its members without any sort of segregation.

Tanzanian Community in Rome counts alot on members monthly contributions in order to keep the community alive.But all in all, it appreciates any sort of contribution from anyone.

Wednesday, June 20, 2012

BALOZI WA TANZANIA NCHINI ITALIA AKABIDHI HATI KWA RAIS WA ITALIA MH GIORGIO NAPOLITANO

Balozi wa Tanzania nchini Italy, Eng. Dr. James Alex Msekela, alikabidhi Hati za utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Italy, Mhe. Giorgio Napoletano, hapo tarehe 19 Juni 2012 saa 11.10 jioni katika kasri ya Rais (Quirinale) iliyopo mjini Rome. Katika hafla hiyo fupi, iliyoanza saa 11 kamili za jioni kwa kwa mapokezi rasmi yaliyohusisha pia gwaride la heshima, Balozi Msekela pia alikuwa na mazungumzo mafupi na mweneyeji wake baaada ya hati zake kupokelewa, ambapo pia alifikisha salaam za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete. Balozi wa Tanzania nchini Italy pia ndiye mwakilishi wetu katika nchi za Ugiriki, Uturuki, Slovenia, Croatia, Serbia, Malta, Bosnia na Herzegovina, na Albania. Katika uwanda wa mashirikiano mapana ya kimataifa, Balozi huyu pia anaiwakilisha Tanzania katika FAO, WFP na IFAD, ambayo yote ni mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) yenye makao yake makuu mjini Rome.

Balozi wa Tanzania nchini Italy, Eng. Dr. James Alex Msekela, akikabidhi Hati za utambulisho kwa Mh. Giorgio Napoletano, Rais wa Jamhuri ya Italy, jana tarehe 19 Juni 2012 saa 11.10 jioni katika kasri ya Rais ijulikanayo kama ‘Quirinale’.



Mh. Giorgio Napoletano, Rais wa Jamhuri ya Italy, akimkaribisha Balozi wa Tanzania nchini Italy, Eng. Dr. James Alex Msekela, katika kasri yake iliyopo kati kati ya mji wa Rome. Kasri hiyo inajulikana kama ‘Quirinale’. Pamoja na Mh. Napoletano, walikuwepo pia; Mkuu wa Itifaki katika kasri hiyo, na washauri wengine wa Rais wa Italy.


Rais wa Jamhuri ya Italy, Mh. Giorgio Napoletano, akipitia Hati za utambulisho wa Balozi wa Tanzania nchini Italy, Eng. Dr. James Alex Msekela. Baadaye Mh. Rais alimkaribisha Balozi ofisini kwake kwa mazungumzo mafupi.


                         Mabalozi wengine waliopeleka hati za utambulisho ni hawa hapa chini!

                               Hon. Alfredo Arosemena Ferreyros, Republic of Perù.


                                                      Hon. Chun Guk Kim, Korea


                                                    Hon. Surapit Kirtiputra, Thailand


                                       Hon. Francisco Javier Elorza Cavengt, Spain.

JUMUIYA YA WATANZANIA ROMA INAUNGANA NA SERIKALI YA ITALIA KWENYE KUMKARIBISHA NA KUMPONGEZA ENG. DR. JAMES MSEKELA NCHINI ITALIA. JUMUIYA YA WATANZANIA ROMA PIA INAAIDI KUSHIRIKIANA NA MH. BALOZI KWENYE MASWALA MBALI MBALI YA KUJENGA TAIFA LETU LA TANZANIA.


                                                        Picha zote na Quirinale, Rome.

No comments:

Post a Comment