Leo tarehe 18 Mei 2012, Watanzania kutoka kila kona ya Roma, wakiongozwa na balozi wa Tanzania nchini Italia, Mheshimiwa James Msekela, pamoja na marafiki mbalimbali wa marehemu James A. Mbwana, walikusanyika kwenye misa takatifu ya kuuaga mwili wa marehemu aliyefariki gafla jumatano tarehe 16 mei 2012 maeneo ya Termini mjini Roma akiwa njiani kuelekea Chuoni kama ilivyokuwa kawaida yake. Misa hii
imefanyika katika parokia ya Mtakatifu Francisco jimboni Palestrina mjini Roma ambako marehemu alikuwa akitumikia na kuishi sambamba na
kufuatilia masomo yake katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino kilichopo mjini Roma. Misa iliongozwa na Mhasham Askofu Dominic, Askofu wa Jimbo la Palestrina.
Habari zaidi juu ya lini mwili wa marehemu utaondoka tutawapatieni kadri tutakapo zipata. Kwa niaba ya Jumuiya ya Watanzania Roma tunawapa pole sana ndugu, jamaa na marafiki kwa msiba huu mkubwa ambao unatukumbusha kuwa sisi binadamu hapa duniani ni wapita njia tu. Siku yoyote mwenyezi Mungu anaweza kutuchukua. Kwa hiyo hatuna budi kujiandaa kwa kusali na kutenda mema mbele ya mwenyezi Mungu.
Bwana ametoa, bwana ametwaa jina lake liidimiwe milele amina!
Bwana ametoa, bwana ametwaa jina lake liidimiwe milele amina!
Jeneza la Marehemu Fr. James Mbwana likiwa kanisani wakati wa misa.
Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mh. James Msekela pamoja na Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Watanzania Roma Mh. Leonce Uwandameno wakati wa ibada takatifu.
Ibada ikiendelea.
Mwili wa Marehemu James Mbwana Ukitolewa kanisani na mapadri wakitanzania. |
Baada ya misa kuisha. |
Mh. Balozi akilonga na Paroko wa parokia aliyokuwa anakaa marehemu.
Picha zote na Fr. Flavian Kassala
No comments:
Post a Comment