Ratiba ya Sherehe ya Muungano wa Jamhuri yaTanzaniaMheshimiwa Balozi akiteta na Mr. Mbilinyi kabla ya kuingia ukumbini.Mh. Balozi akisalimiana na Watanzania kabla ya Kuingia Ukumbini. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Rome Mh. Leonce Uwandameno.Katikati kwa mbali ni Mwenyekiti wa Watanzania Italia Mh. Abdulrahaman A.Alli, na kulia kabisa ni Katibu wa Watanzania Modena ndugu Mwinyimwaka Hatibu.
Mh. Balozi James Msekela akiingia Ukumbini.Mwenyekiti wa Watanzania akielezea mawimi matatu.Katibu wa Watanzania Modena Mh. Mwinyimwaka akielezea maswala mbalimbali yanahusu Watanzania mjini Modena.
Mh. Balozi James Msekela akiingia Ukumbini.Mwenyekiti wa Watanzania akielezea mawimi matatu.Katibu wa Watanzania Modena Mh. Mwinyimwaka akielezea maswala mbalimbali yanahusu Watanzania mjini Modena.
Ukumbi ulipendezeshwa na Watatu wengi.Dj Beka akipozi na Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Roma ndugu Andrew Chole MhellaHivi ni vichache tu ya vingi vilivyokuwepo kwenye sherehe.
Kwa mbali Mama Tandika pamoja na Mama Mhella nao walikuwepo.
Dj. Beka alizungukwa na mashine ya nguvu.
Ile sherehe ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyokuwa ikisubiriwa na wengi mjini Roma, ilifanyika jumamosi tarehe 12 Mei 2012.Sherehe ilifanyika kwenye ukumbi wa Karispera club 69, uliopo katikati ya mji mkuu Roma na kuudhuliwa na Watanzania wengi kutoka sehemu mbalimbali za Italia. Mgeni rasmi alikuwa balozi wa Tanzania nchini Italia, Mh. James Msekela, ambaye kwa mara ya kwanza alikutana na Watanzania kwa pamoja kutoka kila kona ya Italia. Kwenye sherehe hii, balozi Msekela aliishukuru Jumuiya ya Watanzania Roma kwa kuandaa sherehe hii muhimu kwa Taifa la Tanzania kutokana na dhumuni lake la kusherekea muungano ambao ni moja ya ngao ambazo tuliachiwa kama urithi na baba wataifa Mwalimu Julius kambarage Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume. Balozi Msekela pia aliwaelezea Watanzania kuwa amefurahishwa sana na umoja ambao ameuona kwenye siku chache toka kufika kwake nchini Italia na kuwaomba Watanzania waendelee na moyo huu wa ushirikiano maana ndio kitambulisho cha Tanzania nje ya nchi. Balozi alihaidi kushirikiana na hizi jumuiya za Kitanzania hapa Italy na kuwaomba wasisite kwenda kumuona pale watakapo kuwa wanaitaji ushauri na msaada wa aina yeyote toka ofisini kwake.
Mungu Ibariki Tanzania
( Picha na George Mayaka) zingine zitafuata muda si mrefu.
Mungu Ibariki Tanzania
( Picha na George Mayaka) zingine zitafuata muda si mrefu.
No comments:
Post a Comment