Pages

log with Fire

WELCOME TO TANZANIA
Tanzanian Community in Rome, Via GIUSEPPE DI VITTORIO 9, 00067 MORLUPO, Rome, Italy -- Sasa Mnaweza kuweka Michango yenu ya mwezi kwenye account ya Jumuiya: Banki ya Posta:Associazione dei Tanzaniani a Roma Acc. Number 000007564174 Codice Fiscale: 97600810580 ---

welcome to Tanzania

TANZANIAN COMMUNITY IN ROME (TZ-RM,) is a community that unites TANZANIANS living in Rome and those living outside of Rome who have read, understood and accepted the content of its Constitution and hence becoming part of the community's family. Tanzanian Community in Rome is a fruit of the well designed ideas, approved by all community members at the Community's First General Meeting held on the 30th January, 2010. It is a non-political, non-religious, non-ethnical and non-gender based kind of organization. It is a community that democratically, accepts and respects different ideas from all its members without any sort of segregation.

Tanzanian Community in Rome counts alot on members monthly contributions in order to keep the community alive.But all in all, it appreciates any sort of contribution from anyone.

Wednesday, May 16, 2012

BREAKING NEWS: TAARIFA ZA MSIBA MJINI ROMA

UJUMBE KUTOKA KWA KATIBU WA CHAMA CHA WANAFUNZI WATANZANIA WAKATOLIKI ROMA
WAPENDWA WANA UMOJA, TUMSIFU YESU KRISTU!
KWA NIABA YA MWENYEKITI WETU PADRI RICHARD TIGANYA, NA UONGOZI MZIMA TUNAPENDA KUWAPA TAARIFA ZA KIFO CHA GHAFLA CHA MHESHIMIWA PADRE JAMES AMON MBWANA WA JIMBO KATOLIKI LA MBEYA KILICHOTOKEA LEO HAPA ROMA.
MAREHEMU PADRE JAMES ALIKUTWA NA MAUTI ALIPODONDOKA GHAFLA MAENEO YA TERMINI AKIWA NJIANI KWENDA CHUO.
MPENDWA PADRE JAMES ALIKUWA ANAISHI ZAGALORO NA ALIKUWA ANASOMA LUGHA YA KILATINI NA KIGIRIKI CHUO CHA MTAKATIFU AUGUSTINO.
KWA SASA MWILI WA PADRE JAMES UKO KATIKA CHUMBA CHA MAITI NA MAENEO YA TERMINI NA TARATIBU ZINGINE ZINAFANYIKA.
TUNAWAAHIDI KUWAPA TAARIFA ZAIDI ZA NINI KITAFATA HASA SWALA LA KUMUAGA.
RAHA YA MILELE UMPE EE BWANA.......!
PADRE CHRISTIAN LIKOKO
KATIBU

JUMUIYA YA WATANZANIA ROMA IMESIKITISHWA SANA NA KIFO HICHI CHA GAFLA CHA PADRE AMON MBWANA. TUNAWAPA POLE NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI WA MAREHEMU. MWENYEZI MUNGU AMLAZE MAREHEMU PADRI JAMES AMON MBWANA MAHALI PEMA PEPONI AMINA.

1 comment:

  1. .... na mwanga wa milele umwangazie, apumzike kwa amani, Amina.
    Hakika hatujui muda, siku wala saa ... ndiyo maana yatupasa kutendeana mema (UPENDO UTAWALE MAHUSIANO YETU).
    Tutaendelea kusoma kwa taarifa ya misa na mengine. Mungu awaongoze hata mkamilishe hili.

    ReplyDelete