Uchaguzi utaendeshwa kwa kufuata kanuni za katiba.
Vipengele hivyo ndivyo vitakavyo saidia kupata viongozi wapya:
5.1 Sifa za Viongozi
Ili mwanajumuiya aweze kugombea au kuchaguliwa kuwa mmoja wa
viongozi wa jumuiya, atatakiwa awe na sifa zifuatazo:
a) Mwenye kuishi kihalali hapa Italia;
b) Awe hajawahi kushtakiwa kwa kosa lolote la jinai.
c) Awe na uwezo wa kuongoza jumuiya kwa busara;
d) Awe mwaminifu;
e) Wenye kuheshimu na kutunza vifaa mbalimbali vya jumuiya.
5.2 Uchaguzi wa Viongozi
Uchaguzi wa viongozi yaani mwenyekiti, mwenykiti msaidizi, katibu, katibu
msaidizi, mweka hazina na wajumbe wawili, utafanyika kila baada ya miaka
miwili. Lakini pia unaweza kufanyika wakati wowote ambapo mkutano wa
wanajumuiya utaitisha uchaguzi kwa mujibu wa katiba hii.
5.2.1 Baada ya kiongozi mpya kuchaguliwa, kutakuwa na kipindi cha miezi miwili ya
kukabidhi madaraka.
5.3 Uchaguzi wa viongozi utafanyika katika mkutano utakaoudhuriwa na zaidi ya
nusu ya wanajumuiya. Pale ambapo uchaguzi kwa nafasi inayogombewa
unalenga kuwapata washindi zaidi ya mmoja basi washindi watakuwa ni wale
waliopata kura nyingi kuwazidi wengine hadi kupata idadi inayoitajika kwa nafasi
hiyo inayogombewa.
No comments:
Post a Comment