![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhDnFQiBlzhf0SRKxoBynhyphenhyphenY_VKvCo_cCoSgLlmQaC1WOVzQ1ySZ-2G072HWDgRU2TQdscVHXvr1xu93I22iG0TWteAB4oUpTmKZJiWraYCFCjr3k7T2fL2q5N6ng6EUeu5STKFarA5kneu/s400/30-01-2010.jpg)
Hapa ni wakati kujadili katiba, kutoka kushoto ni ndugu Andrew Chole Mhella, katikati ni Mh. Andrew Kyabashasa ambaye alikuwa mwenyekiti wa mkutano wa uchaguzi na kulia ni Mgeni rasmi, Mh. Kaimu balozi Salvator Mbilinyi (Kutoka kwenye Kumbukumbu zetu)
Leo 30 Jan. 2012, Jumuiya ya Watanzania Roma imetimiza rasmi miaka miwili tangu kuanzishwa kwake mnamo 30 Januari 2010. Itakumbubwa na wengi kuwa siku kama leo kwenye ukumbi wa l'aggiustafesta, uliopo mtaa wa via cassalettico 6, eneo la cassia-Grottarossa, Watanzania kwa pamoja walikutana kujadili na kupitisha katiba. Siku hiyo hiyo watanzania hao walifanya uchaguzi wa viongozi ambao kwa kipindi cha miaka miwili wameongoza jumuiya. Kaimu Balozi Mheshimiwa Salvator Mbilinyi alikuwa mgeni rasmi siku hii ya kihistoria ya Watanzania Wahishio Rome. Kwenye mkutano huu Watanzania wafuatao walichaguliwa kuwa viongozi: Mwenyekiti( Leonce Uwandameno); Mwenyekiti Msaidizi(Erasmus Pindu Luhoyo); Katibu ( Andrew Chole Mhella); Katibu msaidizi ( Diana Paul Olotu); Mweka Hazina (Awadhi Suleiman) na Wajumbe (Bwana Boniface Mhella na Bi. Khadija Kirro).
Kulingana kifungu namba 5.2 cha katiba, kila baada ya miaka miwili, wanajumuiya wanapaswa kufanya uchaguzi wa viongozi wapya. Kutokana na viongozi wa sasa kumaliza kipindi chao cha uongozi, kutakuwa na uchaguzi wa viongozi wapya siku chache zijazo. Uongozi utawatambazia pale mipango yote itakapokuwa imekamilika.
Uongozi wa jumuiya unapenda kuwakumbusha watanzania wote kuwa uchaguzi utahusisha WANAJUMUIYA HAI TU. Wanajumuiya hai ni wale ambao wanashiriki kwenye vikao mbalimbali vya jumuiya na ambao wanashiriki kwenye kuchanga michango ya kila mwezi na michango mbalimbali ambayo inaidhinishwa na wanajumuiya wote na wale ambao hawajavunja kanuni za katiba.
Mungu Ibariki Jumuiya ya Watanzania Rome, Mungu ibariki Tanzania.
No comments:
Post a Comment