![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjSIr7CKGcr87zNsrTAAGeaw3DOGJy5ePIdTT9DYoHpqw3p6uDwOCAWZCGH4HXZIicDFGncDHa72hyphenhyphenV5puX-T3qZsiMf0wg3ug_Inxl7IDLDX11jI-dfhMCAKwHRTIahN-QvsMCW_IyOpkx/s400/keki+%25282%2529.jpg)
50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgWoJjvkEV-7XgdQE__WJqGztKgUNIB7Asog6CT3w_hYZMDr3lxarv5FJ51pcMmMLzhBvBGl04nAlK8YDvFNUNabB05qWXBYUUWXIzHf0JlDMrTjCnBQpse7RNjWH0NfUw-8ptNrTdfg7bE/s400/keki3.jpg)
ndugu Andrew Chole Mhella, katibu wa Jumuiya ya Watanzania .
Fungameza wakisakata rumba.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj5GduKWTCbRdwNrVsoTdhddyFmjtwtZ21BUaZtQ8hXSDvG0x628OHpSTPdBRKeuSgGT7rddfL5d2TIxD8OIKRK4S_eZuhic-N_F3wdvHOrRWpgQMJGo4f1lKZ3PVMhKQqcROgZmP7ztFlW/s400/waheshimiwa.jpg)
wa ongera na Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Rome mh. Andrew
Chole Mhella.
na Katibu Andrew Chole Mhella.
wenzake mjini Rome.
Yakubu Kipwate.
Ile sherehe ambayo ilikuwa inasubiliwa na Watanzania wote nchini Italy, ilifanyika siku ya ijumaa tarehe 9 Disemba 2011. Sherehe ilipambwa na Watanzania kutoka sehemu mbalimbali za Italy kama vile Rome, Modena, Napoli, Siena na sehemu zingine na pia kuudhuliwa na wageni kadhaa kutoka nchi rafiki za Tanzania. Mgeni wa heshima alikuwa Kaimu Balozi, Mh. Salvator Mbilinyi ambaye aliambatana na maafisa wote wa ubalozi wa Tanzania nchini Italy. Sherehe ilianza kwa kuimba wimbo wa Taifa na baadae mgeni wa heshima Kaimu Balozi Mh. Salvator Mbilinyi kufungua rasmi. Kaimu balozi alianza kwanza kwa kuelezea umuhimu wa kusherekea siku hii ya miaka 50 ya uhuru. Baada ya hapo alielezea kidogo juu ya upatikanaji wa uhuru wa Tanzania toka kwa wakoloni wa kiingereza. Mh. Kaimu balozi aliwashukuru pia Watanzania wote kwa ushirikiano wao walioonyeshe kwenye kuiandaa siku hii muhimu zaidi viongozi wa Jumuiya mbalimbali za watanzania hapa Italy kwa kuweza kukusanya michango mbalimbali ambayo imeweza kufanikisha sherehe hizi. Mungu Ibariki Africa, Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
No comments:
Post a Comment