![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjmDqvjXUkqHpRrXfYf1v3JTALCYMcGE460E0aFUrPpOiO9VjFmRBd5OKV1lMv4Erysw_gqn_H6FHYIpGm7YK63kKIvSUTjt72do_Qsyj-g7DlLwD1QyQZxhkwimWIi0XUQ1pUb0uqGZkHj/s400/Ukumbi+1.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiNTluFzJc9xR_7XPMvZ0zlb9VwuHTs6209GHgWSEtsh54ciqhc_2LPbNfMO_vLAcs9EeUXeKPDk4CN6XROovYCMW64ioNeugygvVSgDeHSMgIqZBpUklDrS-kPIeD3fwvaqhClfDeYgagh/s400/Ukumbi2.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhLF2rYo3bj8q8nPD6Cgh2-ojlzAYw8cq4ts1khVMsdpJWuDTwKZ6GeqGPdyHq_qnViXsZXiE_DWYdSa0VTYJBo8oVXOG5lJHTIaW3pWwHSNL_THtJVml_yRqCM6mxOnHGZbcG9hLvo4nGH/s400/Ukumbi+3.jpg)
Huu ndio ukumbi (kwa ndani) ambapo sherehe ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika(Tanzania Bara) itafanyika. Sherehe itaanza saa 9 mchama mpaka saa saba usiku. Ukumbi unasehemu mbili, yaani sehemu ya nje na ya ndani. Hapo kwenye picha ni sehemu ya ndani. Kwenye sherehe yetu, tutatumia kumbi zote mbili. Ukumbi wa nje umezungushiwa uzio na kwa juu umefunikwa. Kwa hiyo watu wanaweza kukaa kwa nje bila wasi wasi wa kupigwa na baridi. Nyama choma zitachomewa hapo hapo kwenye Grill la ukumbi ili watu waweze kula nyama choma moto moto.Ukumbi upo kwenye mtaa wa Via Carlo Severini 4. Maelezo ya namna ya kufika yameandikwa kwenye post zilizopita hapo kwa chini. Kwa wale watakao penda kushiriki, mnaombwa kuwasiliana na katibu wa Jumuiya ya Watanzania Rome, ndugu Andrew Chole Mhella kwa e-mail hii, watanzaniaroma@yahoo.it au kwa simu namba 3479094800 au kwa kwenda ubalozini haraka iwezekanavyo.Kwa wale mnaoishi nje ya Rome, mnaweza kuwasiliana na viongozi wa jumuiya zenu kwa maelezo zaidi.Karibuni sana.
No comments:
Post a Comment