Mkutano Mkuu wa jumuiya ya Watanzania Rome ambao uliokuwa unasubiliwa na wengi, jana jioni (19 Nov.)ulifanyika kwenye ukumbi uliopo Via cassalattico 6, maeneo ya Grottarossa-assia.
Mkutano ulianza na wimbo wa Taifa kama desturi ya jumuiya. Baada ya wimbo wa Taifa, wanajumuiya na wageni waalikwa walijitambulisha. Hili ni muhimu haswa kwa sisi tulio nje ya nchi, maana linatuwezesha kufahamiana kwa ukaribu zaidi.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Rome, Mheshimiwa Leonce Uwandameno alifungua mkutano kwa kueleza muhtasari na kisha kumkaribisha katibu wa jumuiya ndugu Andrew Chole Mhella kuelezea mafanikio mbalimbali yaliyotokea kwenye kipindi cha mwaka mzima. Mafanikio ambayo ndugu katibu alielezea ni yafuatayo:
Kwanza kabisa, kwenye kipindi cha mwaka uliopita, Jumuiya ya Watanzania Rome imefanikiwa kuitangaza Tanzania kwa wenyeji wetu hapa Italia. Mafanikio ya kuitangaza Tanzania yalitokana na mikakati kadhaa kama vile jumuiya ilipoandaa SIKU YA UTAMADUNI WA TANZANIA.
Pili, Jumuiya pia ilifanikiwa kushirikiana na jumuiya mbalimbali za Watanzania hapa Italy na zaidi NGOs za kitaliano zinazo fanya kazi nchini Tanzania kwenye maswala mbalimbali.
Tatu, Jumuiya pia inafuraha kuwajulisha pia kwenye mwaka ulioisha imefanikiwa pia kufungua Account ambapo kwa wale ambao hawataweza kufikisha michango yao kwa mweka hazina wanaweza kudeposit michago moja kwa moja kwenye account ya Jumuiya.
katika mkutano wa jana pia kulikuwa kuwe na uchaguzi mkuu wa viongozi wapya kwa mujibu wa katiba. Lakini kutokana na wanajumuiya hai kutofikia idadi inayotakiwa kikatiba, uchaguzi uliahirishwa mpaka hapo itakapotamgazwa tena.

Andrew Chole Mhella,
Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Rome.
No comments:
Post a Comment