Kipengele kilichobadilishwa hapo hawali kilikuwa kinasomeka hivi, "Mchango wa kila mwezi utakuwa ni euro 15, ambazo zinaweza kulipwa kila mwezi au kimafungu ilimradi tu zisicheleweshwe kulipwa zaidi ya miezi mitatu. Wanafunzi wenye miaka chini ya miaka (26) kwenda chini, watapata punguzo la euro 8 na hivyo kutakiwa kulipa euro 7 tu kila mwezi".
Baada ya mabadiliko, kipengele hichi sasa kinasema hivi,"mchango wa kila mwezi utakuwa euro 10 ambazo zinaweza kulipwa kila mwezi au kimafungu ilimradi tu zisicheleweshwe kulipwa zaidi ya miezi mitatu. Wanafunzi wenye miaka chini ya miaka (26) kwenda chini, watapata punguzo la euro 8 na hivyo kutakiwa kulipa euro 7 tu kila mwezi". Wanajumuiya walikubaliana kuwa kipengele hichi kimewekwa kama jaribio kwa kipindi cha mwaka mmoja kuona kama wanajumuiya wataamasika kutochelewesha michango yao ya kila mwezi.
Wanajumuiya kwa pamoja waliafiki pia kuwa, kwa wale wote ambao wanamadeni ya nyuma watatakiwa kuyalipa madeni yao yote kwa kama ilivyokuwa zamani yaani euro 15 kwa kila mwezi.
Andrew Chole Mhella,
Katibu.
No comments:
Post a Comment