
Roma:Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, amefanya yafuatayo kwa heshima ya kanisa la Tanzania:-
1. Ameunda Jimbo Jipya la Kondoa, Tanzania, kwa kumega Jimbo Katoliki la
Dodoma. Kondoa ni moja ya Wilaya kubwa za mkoa wa Dodoma. Jimbo hili jipya
litakuwa chini ya Jimbo kuu la Dar es Salaam. Ikienda sambamba
2. Amemteua Mh. Padre Benardine Mfumbusa wa Jimbo Katoliki la Dodoma kuwa
askofu wa jimbo Jipya la Kondoa. Padre Benardine Mfumbusa ni mzaliwa wa
Arusha.
3. Amemteua pia Mh.Padre John Chrisostom Ndimbo wa Jimbo Katoliki la Mbinga
kuwa askofu wa jimbo Katoliki la Mbinga. Padre John Chrisostom Ndimbo ni
mzaliwa wa Mbinga.
Tumshukuru Mungu kwa neema hiyo na tuwaombee maaskofu hao wateule mara waanzapo utume waweze kulichunga vema taifa la Mungu walilokabidhiwa wakiwa wamejaa Roho wa Mungu.
Kwa habari zaidi waweza kusoma taarifa za leo za redio ya kiswahili ya Vatikani. Mungu awabariki.
Padre Emmanuel Nyaumba
Mtumishi mdogo
No comments:
Post a Comment