





JUMUIYA YA WATANZANIA ROMA, inaungana na Watanzania dunia kote kwenye kuadhimisha kumbukumbu za mwaka wa kumi na moja za kifo cha Baba wa Taifa Letu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Baba wa Taifa ambaye mafunzo yake yamebakia mioyoni mwa kila mtanzania na wapenda amani duniani, alifariki dunia tarehe 14 Oktoba 1999 kwenye ospitali ya Mtakatifu Thomas nchini Uingereza, ambako alikuwa akitibiwa. Kifo cha Baba wa Taifa kimetuachia pengo ambalo alitazibika, ila kitu muhimu kwa sisi Watanzania ni kumuenzi kwa kuyafuata yale ambayo alikuwa anatufundisha. Baba wa Taifa alitufundisha mengi, ambapo mengi yake ndio yamebaki kama msingi wa taifa letu. Itakumbukwa kuwa, Baba wa Taifa alitufundisha umuhimu wa kupendana kama watanzania na kuondoa kabisa ukabila udini na uadui wa aina yeyote ile maana ndivyo huwa ni vyanzo vya mvurugani nchini.
JUMUIYA YA WATANZANIA ROMA, inapenda kuwasihi watanzania kufuata wosia ambao baba wa Taifa alituachia zaidi kwenye mwezi huu wa uchaguzi, ili uchaguzi uwe wa amani na utulivu kama alivyokuwa anapenda Baba wa Taifa.
Watanzania tuishio hapa Rome, na wengine waliotoka sehemu mbalimbali za Italy, miaka ya nyuma (1995) tulibahatika kupata ugeni wa Baba wa Taifa, ambaye alikuja Italy kwaajiri ya kutunukiwa shahada la heshima na kwa upendo wake alitupa fursa ya kukutana nae na kupata chakula cha mchana kwa pamoja kwenye collegio S. Peters licha ya kuwa na ratiba ngumu.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Africa.
No comments:
Post a Comment