Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania Rome unapenda kuwafahamisha wanajumuiya wote kuwa muda si mrefu kamati ya utendaji itakaa ili kuweza kupanga tarehe kamili ya mkutano mkuu wa jumuiya wa kufunga mwaka ambao kulingana na Katiba ni lazima ufanyike kabla mwezi wa Novemba wa kila mwaka kuisha. Kwa wanajumuiya wote ambao wapo nyuma kimchango mnaombwa kujitaidi ili mpaka kufikia tarehe ya mkutano mkuu muwe tayari mmeshakamilisha michango yenu ya mwaka mzima unaokaribia kuisha kikatiba. Jumuiya ya Watanzania Roma, ni jumuiya huru na isiyojiusisha na chama chochote cha siasa hapa Italia au nchini Tanzania. Kuchanganya malengo ya Jumuiya na yale ya kisiasa ni chanzo kikubwa cha kuwachanganya wanajumuiya ambao kila mmoja anamwelekeo wake wa kisiasa lakini ukija kwenye Jumuiya wanamalengo ni yale yale ambao wote tunayafuata kulingana na makubaliano ambayo sote kwa pamoja tulikaa na kukubaliana na si group la watu wachache.
Katibu,
Andrew Chole Mhella
No comments:
Post a Comment