Mwili wa marehemu Hamisi Abdalla George (Mmakua) utasafirishwa kesho (10/08) saa tisa kamili mchana (15:00) kutoka Fiumicino airport (Leonardo Da Vinci) na ndege ya Emirates namba EK098, kupitia Dubai na kuwasili Dar-es-Salaam, Mwalimu Julius Nyerere International Airport jumatano 11/08 saa tisa na dakika ishirini mchana (15:20)na ndege hiyo hiyo ya Emirates namba EK725 na kupokelewa na mwanajumuiya wa Jumuiya ya Watanzania Rome aliyepo kwa sasa mjini Dar-es-Salaam, Tanzania ndugu Andrew Kyabashasa pamoja na ndugu wa marehemu. Jumuiya ya Watanzania Rome inapenda kuwashukuru wanajumuiya wa Jumuiya ya Watanzania Roma ukiongozwa na mwenyekiti msaidizi Mh. Erasmus Luhoyo na Katibu ndugu Andrew Chole Mhella, Napoli ukiongozwa na Mh. Mwandai, Genova ukiongozwa na Mh. Ricky Bondo, Modena ukiongozwa na Mh. Mwinyimwaka bila kuwasahau maafisa wa ubalozi wa Watanzania nchini Italy na marafiki mbalimbali wa marehemu, kwa kujitoa kwa hali na mali kufanikisha shughuli hii ya usafirishaji wa mwili wa marehemu hata pale ambapo mabadiliko ya ghafla ya agency yalipojitokeza. Mungu Ibariki Tanzania, mungu bariki jumuiya zetu zilizopo nje ya Tanzania.
Andrew Chole Mhella,
Katibu wa jumuiya ya Watanzania Roma
No comments:
Post a Comment