Mwenyekiti msaidizi Mh. ErasmuaPindu Luhoyo akielezea ratiba ya kumuaga marehemu.
Imam akiwasili.
Imam akiomba dua.
Picha ya Pamoja ya Viongozi na Wajumbe wa Jumuiya ya Watanzania Rome.
Rome: Watanzania kutoka sehemu mbalimbali za Italia, Jumamosi ya 31/07/2010, walijumuika katika hospital ya Mtakatifu Camillo (San Camilo), mjini Rome, kutoa heshima zao za mwisho kwa Marehemu Hamisi Abdalla George, aliyefariki 18/0 7/2010 baada ya kuugua kwa muda mrefu. Mapema wiki ijayo mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda Dar es Salaam kwa mazishi. Habari Kamili juu ya siku na saa kamili mwili wa marehemu kuwasili nchini Tanzania mtajulishwa mapema iwezekanavyo.
Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania Rome unatoa shukurani za dhati kwa maofisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Italia, Jumuiya za Watanzania Napoli, Genova, Modena na jumuiya ya Mt. Egidio kwa kujitolea kwa ukarimu kwa hali na mali katika msiba huu. Mwenyezi Mungu awajaze maradufu mlichokitoa.
No comments:
Post a Comment